Native Bible

2 Kings 4:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akamwambia mtumishi wake Gehazi, “Mwite huyo Mshunami.” Hivyo akamwita, naye akaja akasimama mbele yake.

2 Kings 4:12 in English

2 Kings 4:12 · Berean Standard Bible

And he said to Gehazi his servant, “Call the Shunammite woman.” And when he had called her, she stood before him,

Context

10Tutengeneze chumba kidogo juu darini na tuweke ndani yake kitanda na meza, kiti na taa kwa ajili yake. Kisha anaweza kukaa humo kila mara akija kwetu.” 11Siku moja Elisha alipofika, akapanda chumbani kwake na kulala humo. 12Akamwambia mtumishi wake Gehazi, “Mwite huyo Mshunami.” Hivyo akamwita, naye akaja akasimama mbele yake. 13Elisha akamwambia mtumishi wake, “Mwambie huyu mwanamke, ‘Umetaabika sana kwa ajili yetu. Sasa utendewe nini? Je, tunaweza kuzungumza na mfalme au jemadari wa jeshi kwa niaba yako?’ ” Akajibu, “Mimi ninaishi kwangu miongoni mwa watu wangu.” 14Elisha akamwambia mtumishi wake, “Je, ni nini kinachoweza kufanyika kwa ajili yake?” Gehazi akasema, “Hakika, hana mwana, na mume wake ni mzee.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.