Native Bible

2 Kings 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku moja Elisha alipofika, akapanda chumbani kwake na kulala humo.

2 Kings 4:11 in English

2 Kings 4:11 · Berean Standard Bible

One day Elisha came to visit and went to his upper room to lie down.

Context

9Akamwambia mumewe, “Ninajua kwamba huyu mtu ambaye anakuja kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. 10Tutengeneze chumba kidogo juu darini na tuweke ndani yake kitanda na meza, kiti na taa kwa ajili yake. Kisha anaweza kukaa humo kila mara akija kwetu.” 11Siku moja Elisha alipofika, akapanda chumbani kwake na kulala humo. 12Akamwambia mtumishi wake Gehazi, “Mwite huyo Mshunami.” Hivyo akamwita, naye akaja akasimama mbele yake. 13Elisha akamwambia mtumishi wake, “Mwambie huyu mwanamke, ‘Umetaabika sana kwa ajili yetu. Sasa utendewe nini? Je, tunaweza kuzungumza na mfalme au jemadari wa jeshi kwa niaba yako?’ ” Akajibu, “Mimi ninaishi kwangu miongoni mwa watu wangu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.