2 Wafalme 25:29
2 Kings 25:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo Yehoyakini akayavua mavazi yake ya mfungwa, na siku zote za maisha yake zilizobaki alikula mezani mwa mfalme.
2 Kings 25:29 in English
2 Kings 25:29 · Berean Standard Bible
So Jehoiachin changed out of his prison clothes, and he dined regularly at the king’s table for the rest of his life.
Context
27Katika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki* alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini kutoka gerezani siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili. 28Alizungumza naye kwa upole na kumpa kiti cha heshima zaidi kuliko wale wafalme wengine aliokuwa nao huko Babeli. 29Hivyo Yehoyakini akayavua mavazi yake ya mfungwa, na siku zote za maisha yake zilizobaki alikula mezani mwa mfalme. 30Siku kwa siku mfalme alimpa Yehoyakini posho siku zote za maisha yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.