2 Wafalme 24:9
2 Kings 24:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akafanya maovu machoni pa Bwana, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.
2 Kings 24:9 in English
2 Kings 24:9 · Berean Standard Bible
And he did evil in the sight of the LORD, just as his father had done.
Context
7Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Frati. 8Yehoyakini alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu. 9Akafanya maovu machoni pa Bwana, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya. 10Wakati huo, maafisa wa Nebukadneza mfalme wa Babeli walikuja ili kuishambulia Yerusalemu, nao wakaizunguka kwa jeshi. 11Nebukadneza mwenyewe akaupandia mji wakati maafisa wake walipokuwa wameuzunguka kwa jeshi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.