2 Wafalme 24:7
2 Kings 24:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Frati.
2 Kings 24:7 in English
2 Kings 24:7 · Berean Standard Bible
Now the king of Egypt did not march out of his land again, because the king of Babylon had taken all his territory, from the Brook of Egypt to the Euphrates River.
Context
5Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 6Yehoyakimu akalala pamoja na baba zake. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake. 7Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Frati. 8Yehoyakini alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu. 9Akafanya maovu machoni pa Bwana, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.