2 Wafalme 19:31
2 Kings 19:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki, na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika. Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote ndio utatimiza jambo hili.
2 Kings 19:31 in English
2 Kings 19:31 · Berean Standard Bible
For a remnant will go forth from Jerusalem, and survivors from Mount Zion. The zeal of the LORD of Hosts * will accomplish this.
Context
29“Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia:
“Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe,
na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake.
Lakini katika mwaka wa tatu, panda na uvune,
panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake. 30Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda
wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu. 31Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki,
na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika.
Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote ndio utatimiza jambo hili. 32“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme wa Ashuru:
“Hataingia katika mji huu
wala hatapiga mshale hapa.
Hatakuja mbele yake akiwa na ngao,
wala kupanga majeshi kuuzingira. 33Kwa njia ile aliyoijia, ndiyo atakayorudi;
hataingia katika mji huu,
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.