2 Wafalme 17:38
2 Kings 17:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Msisahau agano nililofanya nanyi, wala msiabudu miungu mingine.
2 Kings 17:38 in English
2 Kings 17:38 · Berean Standard Bible
Do not forget the covenant I have made with you. Do not worship other gods,
Context
36Bali imewapasa kumwabudu Bwana aliyewapandisha kutoka Misri kwa uwezo wake mkuu na kwa mkono wake ulionyooshwa. Kwake yeye mtasujudu na kwake yeye mtatoa dhabihu. 37Imewapasa daima kuwa waangalifu kutunza hukumu na maagizo, sheria na amri alizowaandikia. Msiabudu miungu mingine. 38Msisahau agano nililofanya nanyi, wala msiabudu miungu mingine. 39Bali, mtamwabudu Bwana Mungu wenu, kwani yeye ndiye atakayewakomboa kutoka mikononi mwa adui zenu wote.” 40Hata hivyo hawakusikiliza, lakini waliendelea na desturi zao za awali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.