2 Wafalme 15:33
2 Kings 15:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alikuwa na miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki.
2 Kings 15:33 in English
2 Kings 15:33 · Berean Standard Bible
He was twenty-five years old when he became king, and he reigned in Jerusalem sixteen years. His mother’s name was Jerusha * daughter of Zadok.
Context
31Matukio mengine ya utawala wa Peka na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 32Katika mwaka wa pili wa utawala wa Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala. 33Alikuwa na miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. 34Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya. 35Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.