2 Wafalme 14:21
2 Kings 14:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha watu wote wa Yuda wakamchukua Azaria* aliyekuwa na umri wa miaka kumi na sita, na kumfanya mfalme mahali pa baba yake Amazia.
2 Kings 14:21 in English
2 Kings 14:21 · Berean Standard Bible
Then all the people of Judah took Azariah,* who was sixteen years old, and made him king in place of his father Amaziah.
Context
19Wakafanya shauri baya dhidi ya Amazia huko Yerusalemu, naye akakimbilia Lakishi, lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi, nao wakamuulia huko. 20Akarudishwa kwa farasi na akazikwa huko Yerusalemu pamoja na baba zake katika Mji wa Daudi. 21Kisha watu wote wa Yuda wakamchukua Azaria* aliyekuwa na umri wa miaka kumi na sita, na kumfanya mfalme mahali pa baba yake Amazia. 22Ndiye aliijenga tena Elathi na kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala pamoja na baba zake. 23Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yehoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala huko Samaria, naye akatawala kwa miaka arobaini na mmoja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.