2 Wafalme 13:9
2 Kings 13:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yehoahazi akalala pamoja na baba zake, akazikwa huko Samaria. Naye Yehoashi* mwanawe akawa mfalme baada yake.
2 Kings 13:9 in English
2 Kings 13:9 · Berean Standard Bible
And Jehoahaz rested with his fathers and was buried in Samaria. And his son Jehoash * reigned in his place.
Context
7Hapakubaki kitu chochote katika jeshi la Yehoahazi isipokuwa wapanda farasi hamsini, magari kumi ya vita na askari wa miguu elfu kumi, kwa kuwa mfalme wa Aramu alikuwa amewaangamiza hao wengine na kuwafanya kama mavumbi wakati wa kupura nafaka. 8Matukio mengine ya utawala wa Yehoahazi yote aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 9Yehoahazi akalala pamoja na baba zake, akazikwa huko Samaria. Naye Yehoashi* mwanawe akawa mfalme baada yake. 10Katika mwaka wa thelathini na saba wa utawala wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yehoashi mwana wa Yehoahazi alianza kutawala Israeli huko Samaria, naye akatawala miaka kumi na sita. 11Alifanya maovu machoni pa Bwana, na hakuacha dhambi yoyote kati ya zile za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, bali aliendelea kuzitenda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.