Native Bible

2 Corinthians 4:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu wala si kwetu.

2 Corinthians 4:7 in English

2 Corinthians 4:7 · Berean Standard Bible

Now we have this treasure in jars of clay to show that this surpassingly great power is from God and not from us.

Context

5Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ingʼae gizani,” ameifanya nuru yake ingʼae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo. 7Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu wala si kwetu. 8Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; 9twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.