Native Bible

2 Corinthians 4:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii kwa rehema za Mungu, hatukati tamaa.

2 Corinthians 4:1 in English

2 Corinthians 4:1 · Berean Standard Bible

Therefore, since God in His mercy has given us this ministry,* we do not lose heart.

Context

1Kwa hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii kwa rehema za Mungu, hatukati tamaa. 2Tumekataa mambo ya siri na ya aibu, wala hatufuati njia za udanganyifu, tukichanganya Neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo, tunadhihirisha kweli waziwazi na kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila mtu mbele za Mungu. 3Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.