Native Bible

2 Corinthians 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea.

2 Corinthians 4:3 in English

2 Corinthians 4:3 · Berean Standard Bible

And even if our gospel is veiled, it is veiled to those who are perishing.

Context

1Kwa hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii kwa rehema za Mungu, hatukati tamaa. 2Tumekataa mambo ya siri na ya aibu, wala hatufuati njia za udanganyifu, tukichanganya Neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo, tunadhihirisha kweli waziwazi na kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila mtu mbele za Mungu. 3Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea. 4Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu. 5Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.