2 Wakorintho 2:9
2 Corinthians 2:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo.
2 Corinthians 2:9 in English
2 Corinthians 2:9 · Berean Standard Bible
My purpose in writing you was to see if you would stand the test and be obedient in everything.
Context
7Basi sasa badala yake, inawapasa kumsamehe na kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi. 8Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwa ajili yake. 9Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo. 10Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu, 11ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.