2 Wakorintho 2:11
2 Corinthians 2:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake.
2 Corinthians 2:11 in English
2 Corinthians 2:11 · Berean Standard Bible
in order that Satan should not outwit us. For we are not unaware of his schemes.
Context
9Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo. 10Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu, 11ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake. 12Basi nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo na kukuta kwamba Bwana alikuwa amenifungulia mlango, 13bado nilikuwa sina utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao nikaenda Makedonia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.