Native Bible

2 Corinthians 12:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, nilijipatia faida kwa kumtumia mtu yeyote niliyemtuma kwenu?

2 Corinthians 12:17 in English

2 Corinthians 12:17 · Berean Standard Bible

Did I exploit you by anyone I sent you?

Context

15Hivyo nitafurahi kutumia kila kitu nilicho nacho kwa ajili yenu, hata mwili wangu pia. Hata ingawa inaonekana ninavyozidi kuwapenda, ndivyo upendo wenu kwangu unavyopungua. 16Iwe iwavyo, kwa vyovyote vile mimi sikuwalemea. Lakini kwa mimi kuwa mwerevu naliwapata. 17Je, nilijipatia faida kwa kumtumia mtu yeyote niliyemtuma kwenu? 18Nilimshawishi Tito aje kwenu, nami nilimtuma pamoja na ndugu yetu. Je, Tito aliwatumia ninyi ili kujipatia faida? Je, hatuenendi kwa roho moja, na hatuchukui hatua zile zile? 19Je, mmekuwa mkifikiri kwamba sisi tunajaribu kujitetea mbele yenu? Sisi tumekuwa tukinena mbele za Mungu kama wale walio katika Kristo. Na chochote tufanyacho, ndugu wapendwa, ni kwa ajili ya kuwatia nguvu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.