2 Wakorintho 11:2
2 Corinthians 11:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Kristo kama mabikira safi.
2 Corinthians 11:2 in English
2 Corinthians 11:2 · Berean Standard Bible
I am jealous for you with a godly jealousy. For I promised you to one husband, to present you as a pure virgin to Christ.
Context
1Laiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo. 2Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Kristo kama mabikira safi. 3Lakini nina hofu kuwa, kama vile Eva alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo. 4Kwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Yesu mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.