Native Bible

2 Chronicles 9:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600*

2 Chronicles 9:15 in English

2 Chronicles 9:15 · Berean Standard Bible

King Solomon made two hundred large shields of hammered gold; six hundred shekels of hammered gold * went into each shield.

Context

13Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,* 14mbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Solomoni dhahabu na fedha. 15Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600* 16Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu* za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni. 17Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.