Native Bible

2 Chronicles 9:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu* za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

2 Chronicles 9:16 in English

2 Chronicles 9:16 · Berean Standard Bible

He also made three hundred small shields of hammered gold; three hundred shekels of gold * went into each shield. And the king put them in the House of the Forest of Lebanon.

Context

14mbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Solomoni dhahabu na fedha. 15Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600* 16Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu* za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni. 17Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. 18Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.