2 Nyakati 9:13
2 Chronicles 9:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,*
2 Chronicles 9:13 in English
2 Chronicles 9:13 · Berean Standard Bible
The weight of gold that came to Solomon each year was 666 talents,*
Context
11Mfalme akatumia hiyo miti ya msandali kuwa ngazi kwa ajili ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa Yuda tangu siku ile.) 12Mfalme Solomoni akampa Malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake. 13Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,* 14mbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Solomoni dhahabu na fedha. 15Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.