2 Nyakati 7:4
2 Chronicles 7:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana Mungu.
2 Chronicles 7:4 in English
2 Chronicles 7:4 · Berean Standard Bible
Then the king and all the people offered sacrifices before the LORD.
Context
2Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Bwana kwa sababu utukufu wa Bwana ulilijaza. 3Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Bwana ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru Bwana wakisema,
“Yeye ni mwema;
upendo wake unadumu milele.” 4Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana Mungu. 5Naye Mfalme Solomoni akatoa dhabihu ya ngʼombe 22,000 pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu. 6Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya Bwana ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu Bwana, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.