2 Nyakati 7:2
2 Chronicles 7:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Bwana kwa sababu utukufu wa Bwana ulilijaza.
2 Chronicles 7:2 in English
2 Chronicles 7:2 · Berean Standard Bible
The priests were unable to enter the house of the LORD, because the glory of the LORD had filled it.
Context
1Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa Bwana ukalijaza Hekalu. 2Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Bwana kwa sababu utukufu wa Bwana ulilijaza. 3Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Bwana ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru Bwana wakisema,
“Yeye ni mwema;
upendo wake unadumu milele.” 4Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.