Native Bible

2 Chronicles 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki.

2 Chronicles 6:3 in English

2 Chronicles 6:3 · Berean Standard Bible

And as the whole assembly of Israel stood there, the king turned around and blessed them all

Context

1Ndipo Solomoni akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene. 2Nimejenga Hekalu zuri kwa ajili yako, mahali pako pa kukaa milele.” 3Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. 4Kisha akasema: “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mikono yake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, 5‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, wala sikumchagua mtu yeyote kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.