2 Nyakati 4:3
2 Chronicles 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja.* Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari.
2 Chronicles 4:3 in English
2 Chronicles 4:3 · Berean Standard Bible
Below the rim, figures of oxen encircled it, ten per cubit all the way around the Sea, cast in two rows as a part of the Sea.
Context
1Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini,* upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.* 2Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini* ingeweza kuizunguka. 3Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja.* Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari. 4Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana. 5Unene wake ulikuwa nyanda nne,* na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 3,000.*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.