Native Bible

2 Chronicles 4:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini,* upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.*

2 Chronicles 4:1 in English

2 Chronicles 4:1 · Berean Standard Bible

He made a bronze altar twenty cubits long, twenty cubits wide, and ten cubits high.*

Context

1Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini,* upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.* 2Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini* ingeweza kuizunguka. 3Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja.* Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.