2 Nyakati 4:2
2 Chronicles 4:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini* ingeweza kuizunguka.
2 Chronicles 4:2 in English
2 Chronicles 4:2 · Berean Standard Bible
He also made the Sea of cast metal. It was circular in shape, measuring ten cubits from rim to rim, five cubits in height, and thirty cubits in circumference.*
Context
1Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini,* upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.* 2Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini* ingeweza kuizunguka. 3Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja.* Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari. 4Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.