2 Nyakati 4:18
2 Chronicles 4:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.
2 Chronicles 4:18 in English
2 Chronicles 4:18 · Berean Standard Bible
Solomon made all these articles in such great abundance that the weight of the bronze could not be determined.
Context
16pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana.
Vitu vyote ambavyo Huramu-Abi alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa. 17Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.* 18Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika. 19Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu:
madhabahu ya dhahabu;
meza za kuweka mikate ya Wonyesho; 20vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya sehemu takatifu ya ndani kama ilivyoelekezwa;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.