Native Bible

2 Chronicles 3:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake.

2 Chronicles 3:2 in English

2 Chronicles 3:2 · Berean Standard Bible

Solomon began construction on the second day of the second month in the fourth year of his reign.

Context

1Ndipo Solomoni akaanza kujenga Hekalu la Bwana katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Bwana alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna,* Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi. 2Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake. 3Msingi aliouweka Solomoni kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa urefu wa dhiraa sitini* na upana dhiraa ishirini.* 4Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini.* Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.