2 Nyakati 3:4
2 Chronicles 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini.* Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.
2 Chronicles 3:4 in English
2 Chronicles 3:4 · Berean Standard Bible
The portico at the front, extending across the width of the temple, was twenty cubits long * and twenty cubits high.* He overlaid the inside with pure gold.
Context
2Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake. 3Msingi aliouweka Solomoni kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa urefu wa dhiraa sitini* na upana dhiraa ishirini.* 4Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini.*
Akaufunika ndani kwa dhahabu safi. 5Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo. 6Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.