Native Bible

2 Chronicles 29:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wa alifungua milango ya Hekalu la Bwana, na kuikarabati.

2 Chronicles 29:3 in English

2 Chronicles 29:3 · Berean Standard Bible

In the first month of the first year of his reign, Hezekiah opened and repaired the doors of the house of the LORD.

Context

1Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. 2Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Daudi baba yake alivyofanya. 3Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wa alifungua milango ya Hekalu la Bwana, na kuikarabati. 4Akawaingiza makuhani na Walawi ndani na kuwakutanisha katika uwanja upande wa mashariki 5na kusema: “Nisikilizeni mimi, enyi Walawi! Jitakaseni nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zenu. Ondoeni uchafu wote kutoka mahali patakatifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.