Native Bible

2 Chronicles 29:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Sasa ninadhamiria moyoni mwangu kuweka Agano na Bwana, Mungu wa Israeli, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nasi.

2 Chronicles 29:10 in English

2 Chronicles 29:10 · Berean Standard Bible

Now it is in my heart to make a covenant with the LORD, the God of Israel, so that His fierce anger will turn away from us.

Context

8Kwa hiyo, hasira ya Bwana ikashuka juu ya Yuda na Yerusalemu, naye akawa amewafanya kitu cha kutisha, cha kushangaza na kitu cha kufanyia mzaha kama mnavyoona kwa macho yenu wenyewe. 9Hii ndiyo sababu baba zetu wameanguka kwa upanga na ndiyo sababu wana wetu na binti zetu, pia wake zetu wamekuwa mateka. 10Sasa ninadhamiria moyoni mwangu kuweka Agano na Bwana, Mungu wa Israeli, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nasi. 11Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa Bwana amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.” 12Ndipo Walawi wafuatao wakaanza kazi: Kutoka kwa Wakohathi, Mahathi mwana wa Amasai na Yoeli mwana wa Azaria; kutoka kwa Wamerari, Kishi mwana wa Abdi na Azaria mwana wa Yahaleleli; kutoka kwa Wagershoni, Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.