Native Bible

2 Chronicles 26:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akamtafuta Mungu katika siku za Zekaria, aliyemwelekeza kumcha Mungu. Wakati wote alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha.

2 Chronicles 26:5 in English

2 Chronicles 26:5 · Berean Standard Bible

He sought God throughout the days of Zechariah, who instructed him in the fear * of God. And as long as he sought the LORD, God gave him success.

Context

3Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na miwili. Mama yake aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 4Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya. 5Akamtafuta Mungu katika siku za Zekaria, aliyemwelekeza kumcha Mungu. Wakati wote alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha. 6Alipigana vita dhidi ya Wafilisti na kubomoa kuta za Gathi, Yabne na Ashdodi. Kisha akajenga upya miji karibu na Ashdodi na mahali pengine katikati ya Wafilisti. 7Mungu akamsaidia dhidi ya Wafilisti na dhidi ya Waarabu walioishi Gur-Baali na dhidi ya Wameuni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.