Native Bible

2 Chronicles 26:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya.

2 Chronicles 26:4 in English

2 Chronicles 26:4 · Berean Standard Bible

And he did what was right in the eyes of the LORD, just as his father Amaziah had done.

Context

2Ndiye alijenga upya Elathi kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala pamoja na baba zake. 3Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na miwili. Mama yake aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 4Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya. 5Akamtafuta Mungu katika siku za Zekaria, aliyemwelekeza kumcha Mungu. Wakati wote alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha. 6Alipigana vita dhidi ya Wafilisti na kubomoa kuta za Gathi, Yabne na Ashdodi. Kisha akajenga upya miji karibu na Ashdodi na mahali pengine katikati ya Wafilisti.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.