Native Bible

2 Chronicles 19:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma.

2 Chronicles 19:5 in English

2 Chronicles 19:5 · Berean Standard Bible

He appointed judges in the land, in each of the fortified cities of Judah.

Context

3Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.” 4Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza wakamrudia Bwana, Mungu wa baba zao. 5Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma. 6Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mtendayo, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili ya Bwana ambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu. 7Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Bwana Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo, wala rushwa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.