Native Bible

2 Chronicles 19:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.”

2 Chronicles 19:3 in English

2 Chronicles 19:3 · Berean Standard Bible

However, some good is found in you, for you have removed the Asherah poles from the land and have set your heart on seeking God.”

Context

1Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu. 2Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukia Bwana? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu ya Bwana iko juu yako. 3Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.” 4Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza wakamrudia Bwana, Mungu wa baba zao. 5Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.