2 Nyakati 18:19
2 Chronicles 18:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye Bwana akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu, mfalme wa Israeli, ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’ “Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile.
2 Chronicles 18:19 in English
2 Chronicles 18:19 · Berean Standard Bible
And the LORD said, ‘Who will entice Ahab king of Israel to march up and fall at Ramoth-gilead?’ And one suggested this, and another that.
Context
17Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu bali mabaya tu?” 18Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama upande wa kulia na wa kushoto. 19Naye Bwana akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu, mfalme wa Israeli, ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’
“Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile. 20Mwishoni, roho akajitokeza, akasimama mbele za Bwana na kusema, ‘Nitamshawishi.’
“Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’ 21“Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’
“Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.