Native Bible

1 Timothy 3:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

(Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe, atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu?)

1 Timothy 3:5 in English

1 Timothy 3:5 · Berean Standard Bible

For if someone does not know how to manage his own household, how can he care for the church of God?

Context

3asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha. 4Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia. 5(Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe, atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu?) 6Asiwe mtu aliyeokoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya ibilisi. 7Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.