1 Timotheo 3:3
1 Timothy 3:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha.
1 Timothy 3:3 in English
1 Timothy 3:3 · Berean Standard Bible
not dependent on wine, not violent but gentle, peaceable, and free of the love of money.
Context
1Hili ni neno la kuaminiwa, kwamba mtu akitamani kazi ya uangalizi, atamani kazi nzuri. 2Basi, imempasa mwangalizi awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha, 3asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha. 4Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia. 5(Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe, atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu?)
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.