1 Wathesalonike 2:7
1 Thessalonians 2:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
lakini tulikuwa wapole katikati yenu, kama mama anayewatunza watoto wake wadogo.
1 Thessalonians 2:7 in English
1 Thessalonians 2:7 · Berean Standard Bible
On the contrary, we were gentle among you,* like a nursing mother caring for her children.
Context
5Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu. 6Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote.
Kama mitume wa Kristo tungaliweza kuwa mzigo kwenu, 7lakini tulikuwa wapole katikati yenu, kama mama anayewatunza watoto wake wadogo. 8Tuliwapenda sana kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu. 9Ndugu zetu, mnakumbuka juhudi yetu na taabu yetu. Tulifanya kazi usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote wa kwenu wakati tulipokuwa tunawahubiria Injili ya Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.