1 Wathesalonike 2:6
1 Thessalonians 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote. Kama mitume wa Kristo tungaliweza kuwa mzigo kwenu,
1 Thessalonians 2:6 in English
1 Thessalonians 2:6 · Berean Standard Bible
Nor did we seek praise from you or from anyone else, although as apostles of Christ we had authority to demand it.*
Context
4Kinyume chake, tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu. 5Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu. 6Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote.
Kama mitume wa Kristo tungaliweza kuwa mzigo kwenu, 7lakini tulikuwa wapole katikati yenu, kama mama anayewatunza watoto wake wadogo. 8Tuliwapenda sana kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.