Native Bible

1 Thessalonians 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu.

1 Thessalonians 2:5 in English

1 Thessalonians 2:5 · Berean Standard Bible

As you know, we never used words of flattery or any pretext for greed. God is our witness!

Context

3Kwa maana himizo letu halikutokana na hila wala nia mbaya au udanganyifu. 4Kinyume chake, tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu. 5Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu. 6Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote. Kama mitume wa Kristo tungaliweza kuwa mzigo kwenu, 7lakini tulikuwa wapole katikati yenu, kama mama anayewatunza watoto wake wadogo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.