1 Samweli 29:5
1 Samuel 29:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, huyu si ndiye Daudi walioimba kumhusu katika ngoma zao, wakisema: “ ‘Sauli amewaua elfu zake, naye Daudi makumi elfu yake’?”
1 Samuel 29:5 in English
1 Samuel 29:5 · Berean Standard Bible
Is this not the David about whom they sing in their dances: ‘Saul has slain his thousands, and David his tens of thousands’?”
Context
3Majemadari wa Wafilisti wakauliza, “Vipi kuhusu hawa Waebrania?”
Akishi akajibu, “Huyu si Daudi, aliyekuwa afisa wa Sauli mfalme wa Israeli? Ameshakuwa pamoja nami kwa zaidi ya mwaka, naye tangu alipomwacha Sauli hadi sasa, sikuona kosa lolote kwake.” 4Lakini majemadari wa Wafilisti wakamkasirikia na kusema, “Mrudishe mtu huyu, apate kurudi mahali pale ulipompangia. Haimpasi kufuatana pamoja nasi vitani, asije akageuka, akawa kinyume chetu vitani. Ni kwa njia ipi bora zaidi angeweza kujipatia tena kibali kwa bwana wake, isipokuwa kwa vichwa vya watu wetu wenyewe? 5Je, huyu si ndiye Daudi walioimba kumhusu katika ngoma zao, wakisema:
“ ‘Sauli amewaua elfu zake,
naye Daudi makumi elfu yake’?” 6Basi Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Kama vile Bwana aishivyo, wewe umekuwa mtu mwaminifu, nami ningependa utumike pamoja nami katika jeshi. Tangu siku ile uliyofika kwangu hadi sasa, sijaona kosa lolote kwako, lakini hao watawala hawakukubali. 7Rudi na uende kwa amani; usifanye chochote cha kuwakasirisha watawala wa Kifilisti.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.