1 Samweli 21:10
1 Samuel 21:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi.
1 Samuel 21:10 in English
1 Samuel 21:10 · Berean Standard Bible
That day David fled from Saul and went to Achish king of Gath.
Context
8Daudi akamuuliza Ahimeleki, “Je, unao mkuki au upanga hapa? Sikuleta upanga wala silaha nyingine yoyote, kwa sababu shughuli ya mfalme ilikuwa ya haraka.” 9Kuhani akajibu, “Upanga wa Goliathi Mfilisti, ambaye ulimuua katika Bonde la Ela, upo hapa, umefungiwa katika kitambaa nyuma ya kisibau. Kama unauhitaji, uchukue, hakuna upanga mwingine hapa ila huo tu.”
Daudi akasema, “Hakuna upanga mwingine kama huo. Nipatie huo.” 10Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi. 11Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema:
“ ‘Sauli amewaua elfu zake,
naye Daudi makumi elfu yake’?” 12Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.