1 Samweli 21:12
1 Samuel 21:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi.
1 Samuel 21:12 in English
1 Samuel 21:12 · Berean Standard Bible
Now David took these words to heart and was very much afraid of Achish the king of Gath.
Context
10Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi. 11Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema:
“ ‘Sauli amewaua elfu zake,
naye Daudi makumi elfu yake’?” 12Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi. 13Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango na kuachia udelele kutiririka kwenye ndevu zake. 14Akishi akawaambia watumishi wake, “Tazameni mtu huyu! Ana wazimu! Kwa nini mnamleta kwangu?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.