1 Samweli 20:18
1 Samuel 20:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo. Itajulikana kwamba haupo kwa kuwa kiti chako kitakuwa hakina mtu.
1 Samuel 20:18 in English
1 Samuel 20:18 · Berean Standard Bible
Then Jonathan said to David, “Tomorrow is the New Moon, and you will be missed if your seat is empty.
Context
16Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi, akisema: “Bwana na awaangamize adui za Daudi.” 17Naye Yonathani akamtaka Daudi athibitishe tena kiapo chake cha kumpenda, kwa sababu Yonathani alimpenda Daudi kama nafsi yake mwenyewe. 18Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo. Itajulikana kwamba haupo kwa kuwa kiti chako kitakuwa hakina mtu. 19Kesho kutwa, inapokaribia jioni, nenda mahali pale ulipojificha wakati tatizo hili lilipoanza na usubiri karibu na jiwe la Ezeli. 20Nitapiga mishale mitatu kando yake, kama kwamba nilikwenda kulenga shabaha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.