1 Samweli 2:12
1 Samuel 2:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wana wa Eli walikuwa watu wabaya kabisa, hawakumheshimu Bwana.
1 Samuel 2:12 in English
1 Samuel 2:12 · Berean Standard Bible
Now the sons of Eli were wicked men; they had no regard for the LORD
Context
10wale wampingao Bwana
wataharibiwa kabisa.
Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni;
Bwana ataihukumu miisho ya dunia.
“Atampa nguvu mfalme wake,
na kuitukuza pembe
ya mpakwa mafuta wake.” 11Kisha Elikana akaenda nyumbani Rama, lakini mtoto akahudumu mbele za Bwana chini ya kuhani Eli. 12Wana wa Eli walikuwa watu wabaya kabisa, hawakumheshimu Bwana. 13Basi ilikuwa desturi ya makuhani pamoja na watu kwamba kila mara yeyote anapotoa dhabihu na huku nyama ikiwa inachemshwa, mtumishi wa kuhani angalikuja na uma wenye meno matatu mkononi mwake. 14Angeutumbukiza huo uma kwenye sufuria au birika au sufuria kubwa au chungu, naye kuhani angalijichukulia mwenyewe chochote ambacho uma ungekileta. Hivi ndivyo walivyowatendea Waisraeli wote waliokuja Shilo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.