1 Samweli 18:9
1 Samuel 18:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuanzia wakati ule na kuendelea Sauli akawa na jicho la wivu juu ya Daudi.
1 Samuel 18:9 in English
1 Samuel 18:9 · Berean Standard Bible
And from that day forward Saul kept a jealous eye on David.
Context
7Walipokuwa wanacheza, wakaimba:
“Sauli amewaua elfu zake,
naye Daudi makumi elfu yake.” 8Sauli akakasirika sana; sehemu hii ya kurudia rudia ya wimbo huu ilimkasirisha sana. Akafikiri kuwa, “Wamempa Daudi makumi elfu, lakini mimi wamenipa elfu tu. Apate nini zaidi isipokuwa ufalme?” 9Kuanzia wakati ule na kuendelea Sauli akawa na jicho la wivu juu ya Daudi. 10Kesho yake roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikaja kwa nguvu juu ya Sauli. Alikuwa akitabiri nyumbani mwake, wakati Daudi alikuwa akipiga kinubi, kama alivyozoea. Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake; 11akautupa kwa nguvu, akijiambia mwenyewe, “Nitamchoma kwa mkuki abaki hapo ukutani.” Lakini Daudi akamkwepa mara mbili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.