1 Samweli 15:32
1 Samuel 15:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Samweli akasema, “Niletee Agagi mfalme wa Waamaleki.” Agagi akaja kwake kwa ujasiri, akifikiri, “Hakika uchungu wa mauti umepita.”
1 Samuel 15:32 in English
1 Samuel 15:32 · Berean Standard Bible
Then Samuel said, “Bring me Agag king of the Amalekites.” Agag came to him cheerfully,* for he thought, “Surely the bitterness of death is past.”*
Context
30Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli; rudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu Bwana Mungu wako.” 31Hivyo Samweli akarudi pamoja na Sauli, naye Sauli akamwabudu Bwana. 32Ndipo Samweli akasema, “Niletee Agagi mfalme wa Waamaleki.”
Agagi akaja kwake kwa ujasiri, akifikiri, “Hakika uchungu wa mauti umepita.” 33Lakini Samweli akasema,
“Kama upanga wako ulivyofanya wanawake
kufiwa na watoto wao,
ndivyo mama yako atakavyokuwa
hana mtoto miongoni mwa wanawake.”
Naye Samweli akamuua Agagi mbele za Bwana huko Gilgali. 34Kisha Samweli akaenda Rama, lakini Sauli akapanda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.