Native Bible

1 Samuel 1:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

naye akamwambia, “Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako.”

1 Samuel 1:14 in English

1 Samuel 1:14 · Berean Standard Bible

and said to her, “How long will you be drunk? Put away your wine!”

Context

12Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake. 13Hana alikuwa akiomba moyoni mwake, midomo yake ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli akafikiri alikuwa amelewa 14naye akamwambia, “Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako.” 15Hana akajibu, “Si hivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa ninaumimina moyo wangu kwa Bwana. 16Usimdhanie mtumishi wako kuwa mwanamke mwovu; nimekuwa nikiomba hapa katika wingi wa uchungu mkuu na huzuni.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.