1 Samweli 1:12
1 Samuel 1:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake.
1 Samuel 1:12 in English
1 Samuel 1:12 · Berean Standard Bible
As Hannah kept on praying before the LORD, Eli watched her mouth.
Context
10Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana. 11Naye akaweka nadhiri, akisema, “Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake.” 12Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake. 13Hana alikuwa akiomba moyoni mwake, midomo yake ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli akafikiri alikuwa amelewa 14naye akamwambia, “Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.